Picha za Chui na Ng’ombe wakiwa katika hali ya utulivu na amani mahali fulani katika maeneo ya mashambani huko Nchini India, zimeendelea kuwashangaza watu wengi ulimwenguni na kuacha simulizi ya hadithi ya kipekee ya mapenzi kati ya marafiki hao wawili, wasiotarajiwa.
Ng’ombe na Chui kwa kawaida si marafiki, kwani wakati mwingine Chui huwawinda Ng’ombe ili kupata chakula, lakini hata hivyo, huwezi hata kujaribiwa kufikiri kwamba unaweza wakuta wakiwa pamoja eti wamepumzika.
Picha hizo zinaowanaonyesha Chui aliyekomaa akicheza na Ng’ombe, ambaye ikiwa maelezo yanayoambatana yanaaminika, yanadai kwamba alimchukua na kumnyonyesha kama mtoto wake baada ya mama yake kufariki na picha ni ushuhuda wa ukweli kwamba miujiza inaweza kutokea.
Ingawa picha zinazozungumziwa zimekuwa zikienea mtandaoni kwa miaka zaidi ya 20 sasa, bado wakati mwingine huwekwa kama habari na kurasa na tovuti zinazotarajia kuzifanya ziwe mtandaoni kwa mara ya bilioni.
Hadithi hiyo mara nyingi huhusishwa na kijiji kisicho na jina huko Assam, wakati ukweli ni kwamba hadithi hiyo ilitokea katika kijiji cha Antoli, jimbo la Gujarat nchini India na chanzo cha kwanza kinaonekana kuwa nakala ya 2002 ilichapishwa kwenye tovuti ya Times of India.
Hadithi asili si ya kutisha kama ile inayopatikana kwenye mitandao ya Facebook, lakini bado ni ya kuvutia na isiyo ya kawaida, kwani Oktoba 2002, maisha ya amani ya wenyeji wa Antoli yalitatizwa na ziara za kila mara za usiku za chui mchanga ambaye alikuwa na tabia isiyo ya kawaidakwani badala ya kutafuta chakula au kushambulia Wanyama wa kufugwa, ilionekana amependezwa na Ng’ombe.
Mara tu baada ya mikutano ya usiku isiyotarajiwa kati ya Ng’ombe na Chui kuzingatiwa na Wanakijiji, umati mdogo ulianza kukusanyika juu ya paa, ili kujionea uchawi huo na katika usiku mwingi, Wanyama hao wawili hawakukatishwa tamaa na macho ya watu.
Ingawa machapisho mengi yanayozunguka mitandao ya kijamii yanadokeza kwamba wanyama hao wawili walifahamiana kwa namna fulani, au hata kwamba Ng’ombe huyo alikuwa amemchukua mtoto wa Chui aliyetelekezwa, chanzo asilia hakitaji chochote kuhusiana na hilo, kwa sababu tu hakuna aliyejua uhalisia.
Hata hivyo, Mhifadhi wa Misitu, H.S. Singh alidokeza tu kwamba huenda chui alikulia karibu na wanadamu na alikuwa akifahamiana na wanyama wa kufugwa akisema, “nyakati nyingine tabia ya wanyama inaweza kurekebishwa,” kauli ambayo aliitoa wakati akihojiwa na Gazeti la Times of India.
Lakini hata kama hadithi hiyo ni ya ukweli, vipi kuhusu Ng’ombe? Kwanini alikubali kukaa karib na Chui? kwani kiasili angeogopa na kukimbia? ila huenda sisi wote hatutawahi kujua hadithi nzima, au jinsi “mapenzi” haya yasiyowezekana yalivyoanza, lakini jambo moja ni hakika, karibu miongo miwili baada ya kuripotiwa awali, hadithi hii bado inavutia mamilioni ya watu.