Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya Nchini – DCEA, imearifu kuwa katika operesheni zilizofanyika mwishoni mwa mwaka 2024, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola walikamata kilogramu 673.2 za methamphetamine na heroin.
DCEA, imearifu kuwa, kati ya dawa hizo kilogramu 448.3 zilizowahusisha raia nane wa Pakistani zilikamatwa Bahari ya Hindi zikiwa zimefichwa ndani ya jahazi lililosajiliwa nchini Pakistani kwa namba B.F.D 16548 huku kilogramu 224.9 zikikamatwa kwenye fukwe za Bahari ya Hindi mkoani Dar es Salaam.
“Kwa mwaka 2024, jumla ya kilogramu 2,327,983.66 za dawa za kulevya zilikamatwa, ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, DCEA imearifu kuwa mafanikio hayo yamewezekana kwa ushirikiano wa vyombo vyote vya ulinzi, wadau wa ndani na nje ya nchi na wananchi kwa ujumla.

Pitcairn: Kisiwa wanachoishi wakazi 50 tu
Malimwengu: Maswali mazito urafiki wa Chui na Ngombe