Kama aumewahi kusikia ama bado basi nakukumbusa kuwa kuna Kisiwa kinaitwa Pitcairn ambacho ndicho kisiwa pekee Duniani chenye wakazi wachache katika Bahari ya Pasifiki Kusini kikiwa kimejitenga na chenye wakazi 50 pekee.

Kipo takriban kilomita 5,300 (maili 3,293) kutoka New Zealand na karibu kilomita 5,500 (maili 3,420) kutoka Amerika Kusini, ambapo kunafanya kuwa moja ya makazi yaliyo mbali zaidi ulimwenguni na ardhi ya karibu yenye Watu, ni ile ya Mangareva katika Polinesia ya Ufaransa, yenye umbali wa takriban kilomita 540 (maili 335).

Kisiwa hiki ni eneo la ng’ambo la Uingereza na wakazi wake hasa wanajumuisha wazao wa waasi wa HMS na wenzao wa Tahiti, ambao waliishi hapo mwishoni mwa karne ya 18 huku maisha ya Pitcairn yakidumishwa na uchumi mdogo wa ufundi, uzalishaji wa asali na utalii.

Wakazi hao wanajinasibu kujitosheleza kiuchumi, ingawa kiuhalisia wanategemea zaidi Meli za robo mwaka kutoka New Zealand ambazo hufika kwa mahitaji muhimu pekee na mandhari yake ni yenye miamba mikali na mabonde yenye majani mabichi, huku kutengwa kwake kukitoa upekee wenye utulivu kwa wakazi wake.

Hakina uwanja wa ndege na njia pekee ya kufikia kisiwa hicho ni kwa kutumia usafiri wa maji ya Bahari, safari ambayo inaweza kuchukua takriban siku mbili kwa boti kutoka Mangareva na kujitenga kwake kunatokana na changamoto za maisha katika mazingira hayo ya umbali wa kisiwa.

Mapenzi ya kweli: Faraja ya mume kituo cha Treni
DCEA waeleza mafanikio udhibiti Dawa za kulevya Nchini