Mwanamke mmoja, Margaret McCollum wa jiji la London Nchini Uingereza kila siku alikuwa akienda kwenye kituo cha Treni ya chini ya ardhi na kuketi, ili kusikiliza tangazo lililorekodiwa na mumewe, Oswald Lawrence aambaye alifariki mwaka 2003.
Huo ulikuwa ni utaratibu wa Margaret, ukilenga kujitafutia faraja ya moyo kwa kumsikiliza mumewe kupitia sauti na kujihisi yu karibu naye licha ya kuwa uhalisia ni kwamba hakuwepo.
Hata hivyo, baada ya miaka mingi kupita, kutokana na mabadiliko ya nyakati tangazo lile lilibadilishwa na Margaret alifadhaika sana, lakini aliomba apatiwe tangazo hilo lile ili akaendelee kusikiliza sauti ya mumewe nyumbani kwake.
Kwa kutambua historia iliyo nyuma ya tangazo hilo, mamlaka ya kituo cha Treni iliamua kurejesha tangazo hilo katika kituo kingine cha jirani na nyumba anayoishi Margaret, lengo likiwa ni kumpatia furaha na kuwakumbusha abiria wengine kuwa mapenzi ya kweli yangalipo.
Mwanabalagha Maundu Mwingizi ambaye tumenakili andiko lake ametuacha swali je, unadhani utakapokufa mpenzi wako atakuweka kwenye wasifu wa Picha kwa muda gani?