Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, George Katabazi amewataka Wanafunzi wa chuo cha Mipango Dodoma kuwa wazalendo na kuepuka kuingia katika makundi hatarishi ya uhalifu na kukatisha ndoto zao na masomo.
Katabazi ametoa kauli hiyo wakati akitoa Elimu ya Ulinzi na Usalama kwa Wanafunzi hao jijini Dodoma na kuahidi kuimarisha ulinzi katika eneo la chuo na maeneo jirani kwa kufanya doria na misako kwa kushirikiana na vikundi vya shirikishi vilivyopo.
Amesema, “Wanafunzi mliojiunga na chuo kwa mwaka wa kwanza pamoja na wanafunzi wengine msiingie katika vishawishi na kuingia katika makundi ya uhalifu.serikali inawategemea katika maendeleo sasa na baada ya kumaliza elimu yenu.”
Hatua hiyo imeufanya uongozi wa Chuo cha na Mipango kulishukuru Jeshi la Polisi kwa kutoa elimu na kuomba Jeshi la Polisi kusogeza huduma ya kituo cha Polisi katika eneo la chuo, ambapo Kamanda Katabazi aliahidi kushughulikia jambo hilo.

Maisha: Mimba tata nyumbani kwa Bosi wangu
Usajili: Wanafunzi Mzumbe watolewa hofu