Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA na Balozi wa Tanzania Nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano.

Akihojiwa hii leo Januari 10, 2025 Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha kushikiliwa kwa Dkt. Slaa akisema yupo katika kituo cha Polisi cha Mbweni.

Amesema, “Daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaiangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza nini cha kufanya na taarifa kamili zitatolewa.”

Dkt. Slaa kupitia mitandao ya kijamii, alisikika akizungumzia kuhusu kukamatwa kwake na Jeshi la Polisi na kwamba anapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mbweni.

Dkt. Biteko: Nishati ya Uhakika inakuza Uchumi wa Nchi
Umeme Nyumba kwa Nyumba: REA yaendelea kuhamasisha Wananchi