Hali mbaya ya uwepo wa baa la njaa nchini Sudani, imeyafanya Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuonya juu ya hatari ya vifo na magonjwa, huku yakidai kuwa watu milioni 12 wameyakimbia makazi yao kutokana na mzozo unaoendelea.

Mashirika hayo, yamearifu kuwa zaidi ya watoto milioni 3 walio chini ya umri wa miaka mitano, wapo katika hatari ya kukabiliwa na utapiamlo mkali katika nchi hiyo yenye vita inayorajiwa kuenea nchi nzima, ambayo ilivyozuka Aprili 15, 2023 kati ya jeshi la Sudani na wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).

Takwimu za UNICEF zinaonesha kuwa takriban watoto 772,000 walio chini ya umri wa miaka mitano wapo katika hatari ya kupata utapiamlo mkali katika mwaka 2026 na watoto 3,200,000 wa rika moja pia wako katika hatari ya utapiamlo mkali.

Aidha, inadaiwa kuwa upatikanaji duni wa huduma za matibabu na maji safi, usafi duni, njia zisizofaa za ulishaji na kuenea kwa uhaba wa chakula ni sababu kuu za kuenea kwa utapiamlo huo mkali.

Nishati Jadidifu: Dkt Kazungu ainadi Tanzania UAE
Ajali ya Ndege yauwa Kenya, wamo waendesha bodaboda