Moto mkubwa mjini Los Angeles Nchini Marekani umesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao ambapo mpaka sasa vifo vimeongezeka na kufikia watu 24.
Mkuu wa kikosi cha zima moto wa Los Angeles, Anthony Marrone amesema upepo mkali unaovuma katika eneo hilo umesababisha eneo hilo kuendelea kuwa chini ya hali ya hatari.
Amesema, kwa wakati huu eneo hilo si salama na hashauri watu kurudi kwenye makaazi yao huku Wazima moto wakiendelea kuudhibiti moto huo ambao umesababisha watu 16 kutojulikani walipo.
Tayari Idara ya utabiri wa hali ya hewa imetahadharisha juu ya kutokea kwa upepo mkali wiki hii, ambao unatabiriwa kuwa huenda ukachochea kuenea zaidi kwa moto huo.