Takriban Watu 11 wamepoteza maisha kwa kugongwa na Lori lenye tela lenye namba za usajili T 680 BQW lililokuwa limebeba saruji, wakati wakiwa barabarani kutoa msaada kufuatia kutokea kwa ajali ya awali ya gari dogo aina ya Tata.

Tukio hilo, limetokea usiku wa kuamkia Januari 14, 2025 katika Kijiji cha Chang’ombe kilichopo Kata ya Segera Wilayani Handeni Mkoani Tanga, baada ya Lori hilo kudaiwa kupoteza uelekeo baada ya mfumo wa wa breki kuharibika.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian ameeleza kuwa mbali na vifo hivyo pia kuna majeruhi 11 wanaoendelea na matibabu, huku miili ya marehemu ikihifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga.

Lema amkataa Mbowe, ataka apumzike amuachie Lissu
DC Kaganda akataa visingizio uhudhuriaji wa msomo Babati