Eva Godwin – Dodoma.

Katika kuelekea siku ya Elimu Duniani ambayo hufanyika kila januari,24, taasisi ya The Living Smile International wameendelea kuunga Mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuandaa Kampeni ya “Utoro sio dili, Shule ni fursa.”

Akizungumza na Dar24 Media Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Venance Kabengwe ambapo amesema lengo likiwa ni kuhamasisha uwandikishwaji na uhudhuriaji wa kudumu mashuleni.

Amesema, “lakini pia lengo la Pili ni kuzielezea fursa mbalimbali ambazo mwanafunzi anaweza akazipata awapo shuleni, tumeona mikakati mbalimbali ya kuanzisha michezo ya aina mbalimbali itakayo wavutia watoto kuhudhuria mashuleni.”

“Kama tunavvyofahamu suala la michezo sahivi limekuwa ni ajira, michezo inaleta umoja, Kwaio ni miongoni mwa mbinu ambazo tutazitumia,” aliongeza Kabengwe

Hata hivyo amesema ipo mikakati ya kupambana na dawa za kulevya kwa Watoto na Vijana waliopo mashuleni kwakuja na kampeni ya “Soma bila stimu” na hii ni kuhakikisha uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali Mashuleni unaendelea kuwanufausha watanzania wa hali zote.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 15, 2025
Wajengewa uwezo kufufua zao la Korosho Pwani