Chama cha Wanasheria Tanganyika – TLS Kanda ya Tabora, kimeburuzwa Mahakamani kwa tuhuma za kukiuka haki ya kikatiba dhidi ya ndugu Mohamed Thabiti Nombo wa mkoani Tabora.

TLS imefikishwa Mahakamani kwa shauri la kesi namba 31308 ya mwaka 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Tabora, Gabriel Ngaeje ambayo imesomwa kwa mara kwanza siku ya Januari 7,  2025.

Shauri la kesi hilo, limefunguliwa na Mohamed Nombo ambaye Chama hicho cha Wanasheria pia kilipeleka malalamiko yake kwa Jaji Mfawidhi Kanda ya Tabora kuhusiana na Nombo kuwa amekuwa akijihusisha na kazi za uwakili kama kuandaa nyaraka za Mahakama, kuingia Mahakamani kuwakilisha wadaiwa kwa kigezo cha kutumia nguvu ya kisheria kinyume na utaratibu wa kisheria.

Shauri hilo kwasasa linasubiri upande wa TLS uweze kujibu tuhuma za malalamiko hayo na limepangwa kutajwa tena Mahakamani hapo siku ya Januari 21, 2025.

Tuhuma za uasi: Rais wa Korea Kusini akamatwa
Maisha: Miaka nane bila kuitwa Mama, nimeshinda