Rais aliyeondolewa madarakani na Bunge nchini Korea Kusini, Yoon Suk Yeol amekamatwa kwa tuhuma za uasi, huku Kiongozi huyo akisema amekubali uchunguzi dhidi yake uendelee ili kuepusha shari. Yoon alionekana katika msafara wa magari akiwasili kwenye ofisi ya idara ya kupambana na ufisadi inayosimamia uchunguzi huo hii leo Januari 15, 2025 majira ya asubuhi na anatarajia kuwa ndani ya saa 48 za kuhojiwa.
Kwa mujibu wa utaratibu, ndani ya muda huo maafisa hao wa upelelezi watatafuta hati ya kuendelea kumshikilia kwa siku 20 zaidi au kumuachia huru Kiongozi huyo ambaye anakuwa ni Rais wa kwanza wa Korea Kusini kukamatwa akiwa madarakani. Mapema hii leo Polisi waliwapeleka maafisa 3,200 kwenye makazi ya Yoon ili kumkamata, lakini mamia ya waandamanaji wanaomuunga mkono na Wanachama wa chama chake cha People Power, walikusanyik

Polisi yawapata Watoto waliopotea kwa Sangoma
Tuhuma ukiukwaji haki ya kikatiba - TLS yaburuzwa Mahakamani