Mkuu wa wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina kupitia hotuba yake iliyosomwa na Afisa Tawala wa Wilayani Buhigwe, Emma Malilo amewataka Madereva bodaboda kufichua wahalifu na vitendo vya uhalifu, ili kuimarisha usalama.

Rai hiyo, imetolewa wakati Madereva bodaboda wapatao 153, walipohitimu mafunzo ya udereva wa udereva wa magari 17 katika Chuo cha VETA wilayani Buhigwe mMkoani Kigoma, ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho.

amesema, VETA Buhigwe inakabiliwa na mwitikio mdogo wa wanabuhigwe ambapo wanaendelea kutoa elimu ya kuhamasisha jamii waje chuoni hapo wapate elimu ya ufundi stadi.

Amesema, Madereva bodaboda hao waliohitimu wapo Madereva bodaboda binafsi na maafisa usafirishaji wanaobeba abiria wa aina mbalimbali katika jamii.

Awali, Mkuu wa Chuo cha VETA Buhigwe Ally Bushiri, amesema kati ya wahitimu hao wa kozi ya udereva bodaboda ni 153, wamehitimu mafunzo ya udereva wa magari 17, mhitimu wa ujenzi mmoja, fundi bomba mmoja, na Kompyuta ni mmoja na Chuo bado kinaendelea na mafunzo kama hayo katika Wilaya jirani zisizo na huduma ya vyuo vya VETA kama wilaya ya Uvinza.

Alitaja aina za kozi fupi na ndefu zilizotolewa tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho mwanzoni mwa mwaka 2024 kuwa ni pamoja na ufundi selemala, udereva wa bodaboda, udereva wa magari, kuchomea, computa, ujenzi, cherehani, udereva wa magari ya abiria.

Amesema, Madereva bodaboda hao waliohitimu wapo Madereva bodaboda binafsi na maafisa usafirishaji wanaobeba abiria wa aina mbalimbali katika jamii.

“Na hao abiria wapo watu wema na wasio wema basi tushirikuane na Viongozi wa serikali tuweze kufichua yale maovu ambayo tutayajua au tutayasikia wakati wakubeba abiria hao.”

Aidha amewataka kuzingatia kanuni, Sheria na taratibu za usalama barabarani na Sheria za nchi katika kuhudumia Wananchi ambazo ni kwa usalama wa abiria wanaowabeba na usalama wao binafsi.

Kwa upande wake Afisa Tawala huyo aliwataka Wananchi wa wilaya ya Buhigwe kutumia Chuo hicho cha VETA kusomesha watoto wao ili kutimiza azima ya serikali kujenga Chuo hicho wilayani humo ili watoto wasiende mbali kufuata huduma ya elimu ya VETA.

“Chuo cha VETA Buhigwe kilianzishwa kwa malengo mazuri ya kusogeza huduma karibu yetu kwani tulikuwa tunahangaika kwenda Kigoma mjini au Kasulu lakini wanabuhigwe tunakwama yaani ukisikia takwimu kuna Wanafunzi 86 kutoka wilaya ya Buhigwe ni sita tu wengine wote ni kutoka wilaya zingine na mikoa mingine.”

Afya Tip: Yafahamu maradhi ya Koo, Tiba sahihi