Amad Diallo ameendelea kuwa shujaa wa dakika za majeruhi kwa Manchester United baada ya kufunga Hat Trick yake ya kwanza akiwa na uzi wa Mashetani hao wekundu. Nyota huyo mwenye miaka 22 na uraia wa Ivory Coast alifunga mabao hayo muhimu dakika ya 82,90 na 90+2 akitokea benchi na kuipa United alama tatu.
Katika mchezo namba 21 kwa Wekundu hao kocha Ruben Amorim alianza na Andre Onana aliyekuwa na kiwango bora kwa kuchomoa michomo mikali ya South Hampton na kuruhusu mabao mawili alisaidiwa na Leny Yoro,De Ligt na Lisandro Martinez kwa eneo la ulinzi . Eneo la kiungo liliundwa na Mazraoui,Kobbie Maino Manuel Ugarte na Amad Diallo.Eneo la mashambulizi liliundwa na Bruno Fernandes,Alejandro Garnacho na Rasmus Hojlund .
Tathmini ya Mchezo
Southhapton walianza kwa kuandika bao la uongozi dakika ya 43 baada ya Manuel Ugarte wa Manchester United kujifunga kwa bahati mbaya na bao hilo kudumu kwa kipindi cha kwanza. Dakika ya 82 Dialo alisawazisha bao hilo na dakika ya 90 na 90+2 akiongeza mawili na kuiofanya United kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Katika mchezo huo kocha Ruben Amorim alilazimika kufanya mabadiliko ya wachezaji watano akliwatoa Kobbie Maino na nafasi yake kuchukuliwa na Antony dakika ya 46.Hojlund akimpisha Zirkzee dakika ya 53 .Manuel akimpisha Collyer .Mazraoui akimpisha Christin Eriksen dakika ya 83 na Lennie Yoro akimpisha Harry Maguire.
Mwenendo wa Manchester United
Manchester United bado haina mwenendo mzuri kwa msimu huu ikiwa nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi na alama 26 pekee. Mbio za ubingwa wa EPL ni kama imejitoa kutokana na kuzidiwa alama 20 na Liverpool viongozi wa ligi. Kwa mwaka 2025 United imecheza mechi 3 ikipata ushindi dhidi ya Arsenal kwa mikwaju ya penati (5-3) baada ya sare ya 1-1 kwenye kombe la FA raundi ya tatu. Sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool mchezo wa raundi ya 20 ligi kuu na ushindi dhidi ya Southhampton.
Katika mechi 3 timu hiyo imefunga mabao 6 na kufungwa mabao 4,tathmini hii fupi inanyesha ni kwa namna gani timu hiyo haina safu nzuri ya ulinzi . Timu hiyo imefungwa mabao 29 katika mechi 21 na kutengeneza deni la mabao 3 kwenye msimamo wa ligi.
Nini kifanyike kuirejesha United katika ubora wake
Kocha Ruben Amorim anakazi ya ziada kuirejesha United katika ukali wake,jambo la kwanza ni kuwatumia kwa usahihi wachezaji wake walioko klabuni hapo ambao baadhi yao wanastahili kuendelea kuvaa jezi ya United .Jambo la pili ni kuwapa mkono wa kwaheri baadhi ya wachezaji ambao wana majina makubwa kama Rashford lakini hakuna walichokifanya kwa misimu hii miwili na lamwisho ni kuingia sokoni na kununua wachezaji wenye vipaji vikubwa na wachanga pasipo kuzingatia gharama zao.
Ubora wa United umeporomoka kwa miaka 12 mfululizo .Kwasasa klabu hiyo imebaki na jina kubwa midomoni na masikioni lakini haina msuli mnene wa kushindana katika sajili za wachezaji wenye kiwango kikubwa duniani.Wachezaji wengi hawaoni sababu za kwenda United kutokana na kukosa mikakati ya uwazi ya kimabadiliko.