Umoja wa Mataifa umesema takribani watu 230,000 wameyakimbia makazi yao huko mashariki mwa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, tangu kuanza kwa mwaka 2025, ili kuepuka ghasia na machafuko yatokanayo na mapigano.

Taarifa ya Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Eujin Byun imeeleza kuwa kuongezeka kwa mapigano kati ya jeshi la Kongo na makundi yenye silaha katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini, kunachochea majanga ya kibinadamu.

Amesema, mgogoro huo unajumuisha vitendo mbalimbali vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kuwalazimisha watu wengi kuyahama makazi yao na kudai kuwa tayari majimbo mawili ya Kivu kaskazini na Kusini yana watu milioni 4.6 waliokimbia makazi yao n kuifanya DRC kuwa moja ya nchi yenye wakimbizi wa ndani katika Dunia.

Hata hivyo, inaarifiwa kuwa Kundi la M23 linalodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda, ambalo linahusishwa na vutendo vya kigaidi na Serikali DRC, limechukua udhibiti wa maeneo mengi mashariki mwa DRC, eneo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali na lililokumbwa na migogoro kwa miaka 30 sasa.

Mgogoro wa ardhi wasababisha kifo cha Bibi kizee Kahama