Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea Urais, aDkt. Samia Suluhu Hassan amempendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025.
Nchimbi ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar, alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023.