Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mtu mmoja amekutwa na maambukizi ya virusi vya Marburg (MVD) Wilayani Biharamuro, mkoani Kagera
Rais Samia anathibitisha uwepo wa ugonjwa huo baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kwamba kuna ugonjwa wa virusi vya Marburg Mkoani humo.
Ameyasema hayo hii leo Januari 20, 2025, wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotembelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Tedros Ghebreyesus Ikulu Chamwino, Dodoma.
Januari 11, 2025 Serikali ilituma timu ya wataalamu mkoani humo na kufanya uchunguzin na katika sampuli zilizochukuliwa ni mgonjwa mmoja pekee aliyekutwa na maambukizi hayo.