Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, imeandaa mchakato wa utoaji elimu ya kisheria kwa kuwafuata Wananchi katika maeneo yao, huku ikiwasisitiza kujitokeza kwa wingi kupata msaada huo.

Hayo yamebainishwa Januari 20,2025 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali,wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na uzinduzi wa wiki ya sheria ambayo huadhimishwa Januari 11 – Februari 1 kila mwaka.

Amesema, siku hiyo huashiria mwanzo wa kuanza kwa shughuli za Mahakama kwa mwaka mpya husika, baada ya kumalizika kwa likizo ya Mahakama inayoanza kila Desemba 15, na kumalizika Januari 31 ya mwaka unaofuata, ili kuanza rasmi utendaji kazi wa utoaji haki.

Jaji Mfawidhi Mahimbali ameongeza kuwa, wiki hiyo kwa Mahakama kuu Kanda ya Shinyanga itazinduliwa rasmi januari 25 na Mkuu wake wa Mkoa katika viwanja vya Zimamoto na itahimishwa rasmi februari 1, 2025 katika Viwanja vya Mahakama Kuu.

Amesema, “kwa kuzingatia maadhimisho ya wiki ya sheria yanafanyika siku za kazi,ambapo wananchi wengi watakuwa kwenye shughuli za utafutaji wa kipato, hivyo utoaji wa elimu kwa mwaka huu umelenga kuwafuata wananchi karibu zaidi na maeneo yao wanayofanyia kazi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.”

“Elimu hii ya kisheria tutaitoa kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi kwa kutumia magari maalumu yatakayokuwa yanahama kutoka eneo moja kwenda jingine,pia tutaongeza wigo wa utoaji elimu kwenye maeneo ya shule za msingi, sekondari na vyuo,” aliongeza Jaji Mahimbali.

Katika maadhimisho hayo, pamoja na mambo mengine itachagizwa na Tamasha kubwa la bonanza la michezo kwa Watumishi wa Mahakama katika ukanda huo ambapo kaulimbiu itakuwa ni “Tanzania 2050 nafasi ya Taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya taifa ya maendeleo.”

Amesema kauli mbiu hiyo inawasaidia kutumia mkakati na ufanyaji wa maboresho ya Mahakama hasa wanapoiendea dira mpya ya matumaini ya mafanikio 2050, ya uchumi wa kiwango cha kati ngazi ya juu, na wao Makahama wamejipanga kufanikisha mpango huo wa maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 – 2050.

Aliyetengeneza picha mjongeo zosizo na maadili adakwa
Maamuzi ya Ancelloti yawaweka njiapanda mashabiki Real Madrid