Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoaji Pwani, kwa akutengeneza picha zisizo na maadili za Wanafunzi wa Shule ya Baobab iliyopo Bagamoyo Mkoani humo.
Kukamatwa kwa mtu huyo kunatokana na uchunguzi wa kitaalam uliosaidia kumfikia mtuhumiwa aliyekutwa akiwa kifaa cha kielektroniki alichokuwa akikitumia kusambaza picha hizo chafu.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani imeeleza kuwa Januari 3, 2025 Jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa Uongozi wa Shule ya Baobaob kuhusu kutengenezwa na kusambazwa katika mitandao ya kijamii picha mjongeo za utupu zenye maudhui machafu kimaadili.
Taarifa hiyo, ilieleza kuwa waliotengeneza waliunganisha na baadhi ya majengo ya shule ya Baobab, ili kuuaminisha umma kuwa vitendo hivyo vinafanyika shuleni hapo, ambapo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limetoa onyo kwa wenye tabia kama hizo kwa malengo ya kuchafua watu au taasisi kuwa mkono wa sheria lazima utawafikia.