Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema miundombinu iliyopo ya kusambaza umeme ni ya muda mrefu na Serikali tayari imeshaanza kazi ya kuibadilisha.
Dkt. Biteko amesema, “miundombinu hii imekuwepo kwa miaka mingi, ndio maana tumeanza kufanya matengenezo kwa kuondoa ya zamani na kuweka mipya.”
Ameongeza kuwa, kazi kubwa imefanyika kwenye kusambaza umeme Vijijini ambapo takribani asilimia 100 ya vijiji vyote vimefikiwa na nishati ya umeme.
Amebainisha kuwa, utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini hivi sasa unaelekea kwenye Vitongoji ambapo kati ya Vitongoji elfu 64 nchini Vitongoji elfu 34 vimefikiwa na nishati ya umeme.
Dkt. Biteko amesema matumizi ya umeme hivi sasa yameongezeka katika sekta nyingine za kiuchumi ikiwemo treni ya SGR, kwenye migodi miku