Napoli inamuwania Alejandro Garnacho, Aston Villa yakataa ombi la West Ham la kumsajili Jhon Duran, Manchester United wako mbioni kumsajili Patrick Dorgu kutoka Lecce na kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anatarajiwa kuondoka majira ya joto.
Napoli wana matumaini ya kufikia mkataba wa pauni milioni 50 kumsaini winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 20. (Corriere dello Sport, kwa Kiitaliano)
Ombi la West Ham la kumsajili Jhon Duran kwa pauni milioni 57 limekataliwa na Aston Villa, ambao wameamua kutomuuza mshambuliaji huyo wa Colombia mwenye thamani ya pauni milioni 80 katika kipindi hiki cha uhamisho wa wachezaji. (Telegraph – usajili unahitajika)
Manchester United wanajadiliana na beki wa Lecce Patrick Dorgu, kwa lengo la kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 20 kuziba pengo katika kikosi cha Ruben Amorim. (Athletic -usajili inahitajika)
United pia imemfuatilia beki wa Wolves na Algeria Rayan Ait-Nouri, 23, na beki wa wa Crystal Palace na England Tyrick Mitchell, 25, kwa kuhofia kumkosa mlinzi wa Paris-St Germain na Ureno Nuno Mendes, 22, katika uhamisho wa wachezaji Januari hii. (ESPN)
Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo majira ya kiangazi, huku kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso akipigiwa upatu kuchukua nafasi ya Muitaliano huyo. (Ondacero – kwa Kihispania)