Nottingham Forest imemfanya mshambuliaji wa Wolves na Brazil Matheus Cunha kuwa shabaha yao kuu ya Januari katika harakati za kufuzu Ligi ya Mabingwa. (Mail)
Arsenal pia wameonyesha nia ya kutaka kumsajili Cunha mwenye umri wa miaka 25 katika uhamisho wa Januari. (Fichajes)
Chelsea wanatazamiwa kufanya mazungumzo zaidi na Manchester United kuhusu winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, ambaye thamani yake ni pauni milioni 50. (Telegraph – usajili unahitajika)
United imemuulizia mchezaji wa Bournemouth na Hungary Milos Kerkez, 21, Wolves na Algeria Rayan Ait-Nouri, 23, na kiungo wa Crystal Palace na Muingereza Tyrick Mitchell, 25, huku kipaumbele cha Ruben Amorim kikiwa kumsajili winga wa kushoto. ( The I)
Chelsea inataka pauni milioni 70 kabla ya kumuachia mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, 27, kujiunga na Bayern Munich. (Sky Sports), nje
Winga wa Manchester United na Brazil Antony, 24, anakaribia kukamilisha uhamisho wa mkopo kuelekea Real Betis. (Sky Sports)
Tottenham na RB Leipzig ndio vilabu viwili vikuu vinavyojaribu kumsajili kiungo wa kati wa Southampton Muingereza Tyler Dibling mwenye umri wa miaka 18. (Sky Germany)
Juventus na Borussia Dortmund zinawania kumsajili beki wa Chelsea na Ureno Renato Veiga, 21, ambaye anaweza kupatikana kwa mkopo au uhamisho wa kudumu. (Times)
Marseille imekuwa klabu ya hivi punde kuonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 27. (L’Equipe)
Hata hivyo Rashford anapigiwa upatu kuelekea Barcelona, kwasababu klabu hiyo imetoa ofa ambayo ingewawezesha kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Athletic -Usajili unahitajika