Ukurasa wa mtandao wa Kijamii wa X wa Freeman Mbowe umechapisha andiko linalothibitisha kuwa Tundu Lissu ameshinda Uchaguzi na kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

“Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu,” ilieleza taarifa ya kurasa hiyo ya Mbowe.

Haya hapa matokeo rasmi ya nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA:

1014 ni zilizojisajili

999 kura zilizopigwa

Kura halali 996

Kura zilizoharibika 3

 

MATOKEO:

Odero Charles kura 1 = 0.1%

Freeman Mbowe kura 482 = 48.3%

Tundu Lissu kura 513 = 51.5%

Nafasi ya mshindi ugombea wa Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara imeenda kwa John Heche ambaye amepata kura 577 akiwashinda wapinzani wake Ezekia Wenje aliyepata kura 372 na Mathayo Gekul aliyepata kura 49.

Tetesi za Usajili Duniani Januari 22,2025
UEFA:Barcelona yatinga 16 bora kwa kishindo