Real Madrid imeendelea kupambania nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya RB Salzburg. Vinicius Jr alirejea kikosini baada ya kukosekana wikiendi iliyopita mchezo wa La Liga dhidi ya Las Palmas. Mchezo huo muhimu uliishuhudia Real Madrid ikicheza kwa kiwango kikubwa na kutengeneza nafasi nyingi zilizotumiwa vyema na Rodrigo,Mbappe na Vini.
Tathmini ya Mchezo
Real Madrid chini ya kocha Carlo Ancelloti walianza na kikosi kilichoundwa na Thibout Couritous,Fredrick Valverde ,Ferran Mendy,Asencio,Rudiger,Luka Modric ,Ceballos,Bellingham,Vinicious,Mbappe na Rodrygo wakitumia mfumo wao wa 4-3-3.
Rodrygo alipachika mabao mawili dakika ya 23 na 34 na mchezo huo kwenda mapumziko Real Madrid wakiwa mbele kwa mabao 2-0. Dakika ya 48 Kylian Mbappe aliandika bao la 3 na Vinicious Juniour akiweka bao la nne na tano dakika ya 55 na 77. Salzburg walipata bao la kufutia machozi dakika ya 88.
Hatua zinazofuata
Ushindi huo umewafanya Madrid kufikisha alama 12 katika michezo 7 waliyocheza wakishika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Uefa. Wababe hao wa Uefa watacheza mchezo wa mwisho dhidi ya Brest siku ya tarehe 29 na kama watashinda mchezo huo watafanikiwa kutinga hatua ya 16 kwa ukamilifu.