Bunge la Iraq, limepitisha rasmi sheria ya kuruhusu watoto wa umri wa miaka tisa kuolewa, hatua ambayo Wanaharakati wamesema itahalalisha ubakaji.

Sheria hiyo mpya inazipa mahakama za Kiislamu mamlaka zaidi katika kushughulikia masuala ya kifamilia ikiwemo ndoa, talaka na mirathi, huku ikiondoa sheria ya awali inayokataza ndoa za watoto walio chini ya umri wa miaka 18 iliyopo toka mwaka 1950.

Waislamu wa Shia ambao ndio wengi zaidi nchini Iraq, sasa umri wa chini zaidi wa kuolewa utakuwa miaka tisa, na wa Sunni, umri rasmi utakuwa miaka 15 kwa mujibu wa Sheria hiyo mpya.

Umoja wa Mataifa – UN kupitia uchunguzi wake unaonesha kuwa suala la ndoa za utotoni limekuwa suala la muda mrefu nchini Iraq, ambapo asilimia 28 ya Wasichana waliolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

NIDA yawatahadharisha Wananchi taarifa feki mtandaoni
Huduma za fedha Vijijini: Serikali yatoa darasa Endabash