Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imeuarifu umma juu ya uwepo wa taarifa inayosambaa katika mitandao ya Kijamii ikiwaeleeza wananchi ambao hawajachukua vitambulisho vyao vya Taifa kubofya na kuingia katika kiunganishi (link) kitu ambacho si cha kweli.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano NIDA, imeeleza kuwa kiunganishi hicho, kinaelekeza kuingia na kuchagaua Mkoa, Wilaya, Kata na kisha Mtaa/Kijiji chake na kwamba ataona Kitambulisho chake kilipo kwasasa na hivyo akakichukue, ujumbe ambao haukutolewa na NIDA.

“Unadhamira ya kuupotosha umma. Kwa sasa NIDA inakamilisha ukusanyaji wa Vitambulisho vyote vilivyokuwa katika Serikali za Kata, Vijiji, Mitaa na Shehia sambasamba na kutuma ujumbe mfupi wa simu kwenda kwa watu waliokuwa hawajachukua vitambulisho vyao kufika katika ofisi za NIDA za Wilaya kuvichukua wakiwa na sms walizotumiwa,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, imearifiwa na Mamlaka hiyo kwamba ni kweli kiunganishi kinachooneshwa kwenye taarifa hiyo inayosambaa ni cha NIDA ambacho kilitengenezwa mwaka 2023 wakati wa zoezi la Usambazaji na Ugawaji mkubwa wa Vitambulisho kwa Umma, kwa lengo la kumpeleka atakaye bofya kiunganishi hicho, kwenye sehemu mahsusi katika tovuti yao, ili kujua Kitambulisho chake kilipopelekwa kwa akati huo aweze kwenda kukichukua.

“Atakeyeona au kupokea taarifa hiyo aipuuze na asubiri apate ujumbe mfupi wa simuutakaomwelekeza kwenda katika ofisi yake ya NIDA ya Wilaya kuchukua Kitambulisho chake,” imibainisha taarifa hiyo.

Serikali yapata ufumbuzi changamoto kivuko cha Kigamboni
Sheria mpya: Watoto wa miaka 9 ruksa kuolewa Nchini Iraq