Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Aliyekuwa Mhasibu Msaidizi katika Zahanati ya Endanachani Wilayani Babati Mkoani Manyara, Mohamed Baya (33) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Babati na kusomewa mashtaka 52 ikiwemo uhujumu uchumi.
Akisoma shauri hilo mbele ya hakimu mkazi mkuu wa mahakama ya wilaya ya Babati Karim Mushi, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Wakili, Martini Makani amesema mshitakiwa na makosa aliyoyatenda kati ya mwaka 2022/2023.
Mwendesha mashtaka Martini Makani, amesema amesema mtuhumiwa huyo alitenda makosa 52 likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha haramu na kugushi nyaraka na kujipatia fedha kwa nyakati tofauti zaidi ya shilingi milioni 48,00,000.
Aidha kesi hiyo imeahirishwa na imepangwa kusikilizwa tena Februari 5, 2025 na mtuhumiwa amepelekwa rumande kwa kuwa kosa la pili la utakatishaji fedha halina dhamana.