Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais -TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Afya la Kimataifa la nchini Korea (KOFIH), Gyeongbae Seo kuhusu namna bora ya utekelezaji na usimamizi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo nchini.
Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dodoma ambapo Dkt. Mfaume amesisitiza ushirikishwaji wa OR- TAMISEMI katika utekelezaji wa miradi, ili watendaji wasimamie na kufanya ufuatiliaji wa kina katika kuhakikisha inaleta tija iliyokusudiwa na mabadiliko chanya katika jamii.
Naye, Mkurugenzi Seo ameipongeza Tanzania kwa ushirikiano wake na kusifu ushirikiano wanaoupata katika utekelezaji wa miradi mbalimbali hapa nchini huku ameeleza uwapo fursa za ufadhili wa miradi ya afya zilizopo nchini Korea na utayari wa nchi hiyo katika kufadhili miradi ya afya nchini Tanzania.
Shirika la KOFIH linatekeleza miradi ya uimarishaji wa huduma za afya ngazi ya msingi katika mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Dodoma.