Chelsea wanafikiria kumsajili winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, baada ya Napoli kusitisha mpango wa kusajilia mchezaji huyo wa Manchester United. (Sky Sports)

Manchester City inavutiwa na beki wa Italia Andrea Cambiaso, 24, lakini Juventus inataka euro milioni 65. (Gazzetta dello Sport – kwa Kiitaliano)

Borussia Dortmund wamejiondoa katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, huku mshahara wa mchezaji huyo wa Manchester United wa pauni 350,000 kwa wiki ukionekana kikwazo. (Mail)

Beki wa Arsenal na Ukraine Oleksandr Zinchenko, 28, anatarajiwa kuondoka kabla ya dirisha la uhamisho wa Januari kufungwa, huku Borussia Dortmund wakimkamia. (Telegraph)

Cambiso

Dortmund pia inamfuatilia beki wa Chelsea na England Ben Chilwell, 28, kama chaguo mbadala. (Sun)

Chelsea imefikia makubaliano ya awali ya kumtoa kwa mkopo kiungo wa Ureno Renato Veiga, 21, kwenda Juventus kwa muda uliosalia. (Athletics)

Beki wa Arsenal na Scotland Kieran Tierney, 27, yuko mbioni kusaini mkataba wa awali wa kurejea Celtic kwa uhamisho wa bure mwishoni mwa msimu huu. (Telegraph)

West Ham wanamtaka mchezaji wa RB Leipzig Andre Silva, 29, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu lakini watamchukua mshambuliaji wa Ajax na Uholanzi Brian Brobbey, 22, ikiwa watashindwa kufikia dili la kumsajili mshambulizi huyo wa Ureno. (Florian Plettenberg)

West Ham wanamfuatilia kiungo wa Uingereza Dan Neil lakini Sunderland wanasita kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuondoka katika msimu huu wa usajili wa wachezaji. (Guardian)

Aston Villa wanataka kusajili mlinzi wa Ufaransa Loic Bade, 24, kutoka Sevilla baada ya kumruhusu beki wa Brazil Diego Carlos, 31, kusajiliwa na Fenerbache. (Express and Star)

Chelsea inamnyatia kiungo wa Hellas Verona na Morocco Reda Belahyane, 20, huku wakijiandaa kummuuza mchezaji wa Italia Cesare Casadei, 22. (Gianluca di Marzio – kwa Kiitaliano)

Beki wa Jamhuri ya Ireland Andrew Omobamidele, 22, anakaribia kuhamia klabu ya Ufaransa ya Strasbourg kutoka Nottingham Forest. (Athletics)

Wolves wamekataa ofa ya awali ya Millwall kwa ajili ya kiungo wa kati wa Uingereza Luke Cundle, 22, ambaye pia anasakwa na Swansea na Bristol City. (Express and Star)

Manyara: CCM waunga mkono maamuzi ya Mkutano mkuu
Maisha: Kama mume wako ni bahili soma hapa