Julian Nagelsmann ameongeza mkataba wake kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani hadi Euro 2028, kama ilivyothibitishwa na Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) Ijumaa.
Rais wa DFB Bernd Neuendorf alionyesha imani na uwezo wa Nagelsmann, akisema, “Julian Nagelsmann anatimiza jukumu lake kikamilifu, shukrani kwa umahiri wake wa michezo na usikivu wake kwa ‘Mannschaft’ na mashabiki.”
Tangu achukue usukani Septemba 2023, Nagelsmann mwenye umri wa miaka 37 ameiongoza timu ya taifa katika mechi 19, zikiwa na mechi nane za kirafiki na mechi 11 za ushindani, zikiwemo michuano iliyopita ya Euro 2024 ilikayoandaliwa nchini Ujerumani na Ligi ya Mataifa.
Katika kutafakari juu ya muda wake wa uongozi, Nagelsmann alibainisha, “Maoni makubwa tunayopokea yanaonyesha tuko kwenye njia sahihi, na bado haijakamilika. Kwa pamoja, mashabiki, timu na wafanyakazi wameunda kitu ambacho tunalenga kuendeleza kwa mafanikio. ; tunataka kushinda mataji.”
Akiwa amejenga taaluma yake nchini Ujerumani, Nagelsmann amewahi kuwa kocha wa Hoffenheim, Leipzig, na Bayern Munich.