Klabu ya KMC FC imeendelea kujiimarisha zaidi msimu huu baada ya kutangaza usajili wa golikipa mpya Ali Ahamada. Nyota huyo ametambulishwa rasmi na klabu hiyo kama mchezaji wa mkopo kutoka Azam FC na taarifa za ndani zinasema atakuwa klabuni hapo mpaka mwish0ni mwa msimu.

Pendekezo la usajili huo linatoka kwa kocha mkuu wa klabu hiyo Kali Ongala . Kocha huyo anaamini Ahamada ni mtu sahihi kwa klabu hiyo kwa kuwa ni mzoefu na uwezo mzuri. Ikumbukwe Kali Ongala ameshawahi kufanya kazi na Ahamada msimu wa 2022/23 walipokuwa Azam FC.

KMC imemsajili kipa huyo kutokana na mwenendo mbaya wa safu ya ulinzi ambayo imeruhusu mabao 21 kwenye mechi 16 walizocheza kwa raundi ya kwanza ya ligi kuu. Uwepo wa Ahamada unaweza kurejesha ari ya ushindani klabuni hapo baada ya kutofanya vyema mzunguko wa kwanza wa ligi wakishinda michezo 5 sare 4 na kupoteza mechi 7.

Kipi kimemtoa Ahamada AZAM FC 

Kwa misimu miwili mfululizo Ali Ahamada hajaonyesha kiwango bora kama ilivyotegemewa ndani ya Azam fc .Ujio wa Zuberi Foba na Mohammed Mustafa ulimfanya nyota huyo kutokuwa na uhakika wa nafasi ndani ya wanachamazi na ikamlazimu kukaa nje kwa muda mrefu hali iliyohatarisha nafasi yake katika kikosi cha timu yake ya Taifa Comoro.

 

 

 

Waziri Kombo ateta na Waziri wa Uchukuzi Czech
Mrithi wa Flick amepewa dili jingine Ujerumani