Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amefanya mazungumzo na Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Czech, Ing. Martin Kupka jijini Prague.

Waziri Kombo alisema sekta ya uchukuzi ni moja ya sekta muhimu katika maendeleo ya nchi na anaona sekta hiyo ina nafasi kubwa ya kupiga hatua kupitia ushirikiano na Czech.

Wamesisitiza umuhimu wa mataifa yao kusaini Mkataba wa anga ili kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja baina ya nchi zao ili kuinua biashara, utalii na mwingiliano wa watu.

Waziri Kombo alipongeza kazi nzuri inayofanywa na kampuni ya Czech ya Airplane Africa Limited inayotengeneza ndege aina ya Skyleader – 600 mkoani Morogoro.

Utengenezaji wa ndege hizo utasaidia kwa kiasi kikubwa kukua kwa sekta ya usafiri wa anga, kuongeza nafasi za ajira na kuimarisha sekta ya utalii nchini.

Waziri Kombo alipongeza pia kampuni ya Skoda Electric kwa kufunga mfumo wa umeme wa kisasa kwenye uendeshaji wa reli ya SGR nchini.

Dhoruba: Wavuvi 540 waokolewa Ziwa Rukwa
KMC yatangaza usajili bora zaidi dirisha dogo