Saulo Steven, Babati – Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amefungua kikao cha maboresho ya kodi Mkoa wa Manyara, kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya kodi Balozi Ombeni sefue.
Kikao hicho kilihudhuriwa na makundi mbalimbali ikiwemo Wafanyabiashara, Wajasiriamali, Taasisi mbalimbali za binafsi na serikali pamoja na zile zinazahusika na kusimamia wafanyabiashara na walipa kodi Mkoa wa Manyara.
Akifungua kikao hicho RC Sendiga, amewataka wafanyabiashara kutoa maoni yao, kero, changamoto na mapendekezo kwa tume hiyo ili waweze kuisaidia Serikali na Mamlaka husika wakati wa ukadiriaji na ukusanyaji wa kodi katika kuleta tija na manufaa yao na taifa kwa ujumala.
Wakitoa maoni yao, Wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa Kodi Mkoani Manyara wameiomba Serikali kuboresha mifumo mbalimbali ya Kodi ambayo ni kandamizi kwakua inarudisha Maendeleo ya Uwekezaji kwenye Sekta ambazo zinahitaji kulipa Kodi kwa hiyari ili kukuza Pato la Taifa.
kwa upande wake Mwenyekiti wa tume ya maboresho ya kodi, Balozi Ombeni Sefue na tume nzima wameweza kupokea maoni, changamoto na mapendekezo yaliyotolewa na wafanyabiashara hao na kuahidi kufanyia kazi mapendekezo hayo kama ilivyo dhumuni la kikao hicho.