Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 25 2025 atazindua Kanzidata na Mfumo wa Taarifa za Watu Wenye Ulemavu Unaotokana Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma
Mfumo huo utawezesha wadau wa maendeleo, na watunga sera katika kupanga, kutekeleza, na kufuatilia maendeleo ya Watu Wenye Ulemavu Nchini.
Pia, Takwimu zilizoandaliwa zinatoa taarifa za msingi ikiwemo idadi ya watu wenye ulemavu kwa jinsi na umri, aina ya ulemavu, kiwango cha elimu na aina ya shughuli za kiuchumi wanazojishughulisha nazo.