Aston Villa wamejiunga na mbio za kumsaka mshambuliaji wa Wolves na Brazil Matheus Cunha, 25, ambaye pia anazivutia Nottingham Forest , Chelsea , Arsenal , Tottenham na Manchester United (Mirror)

Manchester United watatoa ofa ya pili kwa Lecce kwa ajili ya kumnunua beki wa Denmark Patrick Dorgu, 20, baada ya dau lao la pauni milioni 25 kukataliwa. (Fabrizio Romano)

h

Jaribio la Barcelona kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford, 27, huenda likapingwa kwa kuwa hawajauza wachezaji wa kutosha ili kupata pesa. ( ESPN)

West Ham wameambiwa watahitaji kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Brian Brobbey, 22, kwa mkataba wa kudumu kwani Ajax hawana nia ya mkopo. ( Fabrizio Romano)

h

Meneja wa Manchester United ruben Amorim amesikitishwa na klabu hiyo kutokuwa na shughuli ya uhamisho, huku kukiwa hakuna mchezaji aliyenunuliwa au kuuzwa mwezi huu. ( (Manchester Evening News)

Klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia inatayarisha ofa rasmi kwa ajili ya mshambuliaji wa Aston Villa na Colombia Jhon Duran, 21. ( Telegraph -subsctription is required)

g

Mchezaji wa Manchester United Alejandro Garnacho atajiunga na Chelsea mwezi huu baada ya mazungumzo ya winga huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 kuhusu kuhamia Napoli kukwama. (Teamtalk)

Real Madrid wameanza mazungumzo ya awali na kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Joshua Kimmich, 29, kuhusu uhamisho wa majira ya joto, mkataba wake utakapomalizika. (Bild – subscription is reguired)

g

Arsenal haijapokea ofa zozote za kumnunua mchezaji Oleksandr Zinchenko, 28, licha ya kupatikana kwake kwa mauzo. ( Sky Sports )

Atletico Madrid wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine, ambaye anaweza kucheza katika safu ya ulinzi au kiungo, lakini Borussia Dortmund wamepunguza nia yao. ( Sky Sports)

Brighton wanafikiria iwapo watamruhusu mshambuliaji Evan Ferguson, 20, kuondoka kwa mkopo mwezi huu na vilabu vingine vingi vya Primia Ligi) vinavyomtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland. ( Mirror)

h

Barcelona wanamfuatilia mlinzi wa Nottingham Forest Murillo, huku Juventus na Chelsea pia wakimtaka Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 22. (Sport – in Spanish)

Chelsea wamekataa ofa ya £8m kwa ajili ya winga wa Deportivo La Coruna na kikosi cha vijana wenye umri wa chini ya miaka 21 cha Uhispania Yeremay Hernandez.

Mshambulizi wa Ipswich Ali Al-Hamadi, 22, amekamilisha vipimo vya afya huko Stoke kabla ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Iraq kujiunga kwa mkopo kwa msimu uliosalia. ( Sky Sports)

h

Aston Villa inapanga kumnunua mshambuliaji wa Besiktas na Uturuki Semih Kilicsoy, 19, kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho. (Football Insider)

Atalanta wamedhamiria kumshikilia mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27, huku kukiwa na tetesi kwamba anaweza kurejea Ligi Kuu. (Corriere della Sera – in Italian)

Jina la KOLO laanza kuimbwa Italy,Mashabiki wapata tumaini jipya
Ugeni mzito Tanzania: Baadhi ya barabara kufungwa - Chalamila