Aston Villa wamejiunga na mbio za kumsaka mshambuliaji wa Wolves na Brazil Matheus Cunha, 25, ambaye pia anavutia Nottingham Forest, Chelsea, Arsenal, Tottenham na Manchester United. (Barua)
Jaribio la Barcelona kumsajili fowadi wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford, 27, huenda likapingwa kwa kuwa hawajauza wachezaji wa kutosha ili kupata pesa. (ESPN,)
Manchester United watatoa ofa ya pili kwa Lecce kwa ajili ya kumnunua beki wa Denmark Patrick Dorgu, 20, baada ya dau lao la pauni milioni 25 kukataliwa. (Fabrizio Romano)
Meneja wa Manchester United Ruben Amorim amesikitishwa na klabu hiyo kwa kutokuwanunua wachezaji mwezi huu. (Manchester Evening)
Klabu ya Saudi Arabia Al-Nassr inatayarisha ofa rasmi kwa ajili ya mshambuliaji wa Aston Villa na Colombia Jhon Duran, 21. (Telegraph – Subscription Required).
West Ham wameambiwa watahitaji kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Brian Brobbey, 22, kwa mkataba wa kudumu kwani Ajax hawana nia ya kumtoa kwa mkopo. (Fabrizio Romano)
Real Madrid wameanza mazungumzo ya mapema na kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Joshua Kimmich, 29, kuhusu uhamisho wake, mkataba wake utakapomalizika. (Bild – Subscription Required)
Mchezaji wa Manchester United Alejandro Garnacho atajiunga na Chelsea mwezi huu baada ya mazungumzo ya winga huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 kuhusu kuhamia Napoli kukwama. (TeamTalks)
Everton wanatumai kumtuma mshambuliaji wa Albania Armando Broja, 23, kurudi Chelsea ili kubadilishana naye kwa mkopo kutoka Stamford Bridge, huku viungo wa kati wa Uingereza Kiernan Dewsbury-Hall, 26, na Carney Chukwuemeka, 21, wakiwa kwenye orodha ya David Moyes. (Guardian)
Arsenal haijapokea ofa zozote za kumnunua Oleksandr Zinchenko, 28, licha ya kuwa mchezaji huyo anauzwa. (Sky Sports, nje)
Atletico Madrid wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine, ambaye anaweza kucheza katika safu ya ulinzi au kiungo, lakini Borussia Dortmund wamepunguza nia yao. (Sky Sports, nje)
Brighton wanafikiria iwapo watamruhusu mshambuliaji Evan Ferguson, 20, kuondoka kwa mkopo mwezi huu huku kukiwa na vilabu vingi vya Ligi ya Premia vinavyomtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland. (Mail)
Chelsea imekataliwa dau la pauni milioni 8 kwa ajili ya winga wa Deportivo La Coruna na Uhispania U21 Yeremay Hernandez, 22. (Fabrizio Romano).
Mshambulizi wa Ipswich Ali Al-Hamadi, 22, amekamilisha uchunguzi wa kimatibabu huko Stoke na mchezaji huyo wa kimataifa wa Iraq anatarajiwa kujiunga kwa mkopo kwa muda wote uliosalia. (Sky Sports)
Barcelona wanamfuatilia mlinzi wa Nottingham Forest Murillo, huku Juventus na Chelsea pia wakimtaka Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 22. (Sport – In Spanish)
Aston Villa inapanga kumnunua fowadi wa Besiktas na Uturuki Semih Kilicsoy, 19, kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho. (Football Insider)
Gwiji wa Liverpool Robbie Fowler ametuma ombi la kuajiriwa nafasi ya ukocha iliyo wazi katika klabu ya Bolton, baada ya kuondoka kwa Ian Evatt. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Leicester City Hamza Choudhury yuko mbioni kujiunga na Sheffield United kwa mkopo. (Subscription Required )
Sheffield Wednesday wanamfuatilia mshambuliaji wa Nottingham Forest Emmanuel Dennis, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria akihangaika kwa muda wa mechi. (Sheffield Star, nje)
Maksym Talovierov anafuatiliwa na Plymouth Argyle. Mkataba wa kudumu unatafutwa kwa ajili ya beki huyo wa Ukraine, anayechezea LASK ya Austria. (Dominik Schneider kwenye X,)
Luton wanazidisha nia yao ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa St Gallen Willem Geubbels. The Hatters wanatafuta mkataba wa mkopo kwa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23. (Football League World}
Atalanta wamedhamiria kumshikilia mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27, huku kukiwa na uwezekano wa kurejea Ligi Kuu. (Corriere della Sera – In Itali)
Southampton wamewasilisha dau la pauni milioni 2 kwa ajili ya beki wa Reading Andre Garcia. Zabuni ya kwanza ya Watakatifu kwa kijana huyo wa miaka 17 ilikataliwa wiki iliyopita. (Fabrizio Romano)
Mshambulizi wa Stoke City Niall Ennis anaonekana kwenda kujiunga na Blackpool kwa mkopo huku ‘makubaliano ya mdomo’ yakiafikiwa. (Wrld Football League)
Klabu ya Crewe Alexandra imekataa ofa mbili za kumnunua nahodha Mickey Demetriou kutoka MK Dons. (World football League}.