Hatimaye siku maalumu iliyokuwa ikisubiriwa na wanasoka Barani Afrika imewadia,Leo ni Droo ya kupanga makundi ya timu 16 zitakazoshiriki michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco. Tanzania ni moja ya nchi hizo 16 shiriki tukijivunia ubora wa Taifa Stars chini ya Kocha Hemed Moloko. Taifa Stars inakwenda kushiriki michuano hii kwa mara ya nne. Chini ya Rais Wallace Karia Stars imeshiriki michuano ya AFCON mara ya tatu mfululizo tangu mwaka 2019,2023 na sasa 2025
Wengi tunatamani kuiona Taifa Stars ikirejea na Kombe au Medali kutoka Morocco mwaka huu na tunaamini inawezekana kutokana na weledi wa wachezaji tulionao. Swali jepesi kwa wapenda soka ni je tufanye nini kufikia malengo hayo? Hapa nimekuwekea mabakuli (POTS) nne ambazo zimesheheni washindani wa Stars na lazima watakutana na wapinzaniwa kutoka Pot 1,Pot 2,Pot 3
Pot 1
Pot 2
Pot 3
Pot 4
Afisa Habari wa Yanga ,Ali Kamwe yupo nchini Morocco kushiriki upangaji wa Makundi hayo na leo atashiriki tukio hilo Mahususi litakalofanyika majira ya saa 12 jioni. Africa Mashariki imetoa timu mbili pekee ambazo ni Tanzania na Uganda. Ushiriki wa Timu hizo unakwenda kuongeza thamani ya ukanda wa CECAFA. Ukanda wa SADC unawakilishwa na Zimbabwe,Botswana,Comoro,,Msumbiji,Zambia,Angola,Dr Congo na Afrika Kusini