Rais wa Benki ya Dunia, Ajay Banga amesema asilimia 80 ya ajira duniani huundwa na biashara ndogo na za kati pamoja na wakulima wadogo,

Banga ameyasema hayo hii leo Januari 27, 2025 katika Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika, unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Amessma, “si kutoka kwa makampuni makubwa. Wanahitaji kuandaliwa mazingira ya kufanikisha mafanikio yao, na hilo linahitaji sera bora za udhibiti pamoja na upatikanaji sahihi wa mtaji.”

Pamoja na mambo mengine, pia Mkutano huo unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika na kupitisha Azimio la Dar es Salaam.

Azimio hilo, linalosisitiza dhamira ya viongozi wa nchi na Serikali za Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu na endelevu.

Ngorongoro yaandaa diko la Amboni kung'arisha Valentine
Kocha mkongwe wa Liverpool na Real Madrid hana muda wa kustaafu kwa sasa