Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema suala la Nishati ni msingi muhimu kwa uchumi na jamii duniani.
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo katika Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika, jijini Dar es Salaam hii leo Januari 27, 2025.
Amesema, “tunaweza kudhani ni jambo la kawaida. Fikiria maisha bila nishati kwa siku moja, mwezi mmoja, au mwaka mmoja. Kwa baadhi ya jamii, hali hii haiwezi kufikirika.”
Mwigulu ameongeza kuwa, upatikanaji wa nishati ya uhakika na nafuu unaweza kuchochea ukuaji wa uchumi, kuunda ajira, na kuwawezesha wananchi.
Mkutano huo unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika.