Swaum Katambo – Katavi.

Wataalam wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Wadau wa Stendi kuu ya mabasi ya Mizengo Pinda pamoja na TAKUKURU Mkoa wa Katavi wamekubaliana kuwa wananchi wote wanaoingia katika stendi hiyo kuingia na shilingi 500 kamili, ili kuondoa usumbufu wa upatikanaji wa chenji hali inayosabisha Halmashauri kukosa sehemu ya mapato.

Hayo yamebainisha na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi, Stuart Kiondo wakati akitoa taarifa ya robo ya pili inayoanzia Oktoba hadi Desemba 2024 kwa Waandishi wa Habari baada ya kubaini mfumo wa ukusanyaji wa mapato usio sahihi katika stendi hiyo kutokana baadhi ya watu wanaoingia kutolipia fedha ya ushuru kwa kigezo cha kutoa fedha kubwa na kukosa chenji.

Katika hatua nyingine TAKUKURU Mkoa wa Katavi imefanikiwa kurejesha fedha kiasi cha shilingi laki nane kwa mfugaji mkazi wa Kata ya Kasokola baada ya Takukuru kushinda kesi dhidi ya mtendaji wa Kijiji cha Kasokola ambae alipokea fedha hiyo kama hongo, ili kuachia Ng’ombe wa mfugaji huyo waliokamatwa wakiwa Katika Pori la Hifadhi la North East lililopo katika Kata ya Urwila, Halmshauri ya Nsimbo.

Aidha Kiondo ametoa wito kwa baadhi ya watu wanaotaka kutia nia kwenye uchaguzi ujao na kuanza kutoa rushwa za aina mbalimbali kwa wananchi kufuata utaratibu huku akisema kuwa endapo watabainika watakaoikuka hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.

PPRA, ZPPDA kuendeleza ushirikiano uboreshaji sekta ya ununuzi
Sakata la uraia kwa wachezaji wa Singida Big Stars laibua mapya