Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimearifu kusikitishwa na kauli za kufedhehesha na kutweza utu wa Mwanamke, nyingine zakutatanisha zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa umma kinyume namaadili na miiko ya utumishi wa umma.

Taarifa iliyotolewa na kituo hicho kupitia kwa Mkurugenzi wake Dkt. Anna Henga imeeleza kuwa,kauli hizo pia zipo kinyume na haki za binadamu na misingi yautawala bora.

“Ndugu waandishi wa habari,Mwishoni wa juma lililopita ilisambaa picha mjongeo kupitia vyombo vyahabari ikimnukuu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ndugu Albert Chalamila, wakati akihutubia wananchi katika moja ya hafla wilayani Temeke jijini Dar es Salaam,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, imeeleza kuwa, katika video hiyo, Chalamila alionekana akisema kuwa alipokea malalamiko kutoka kwa mama mmoja aliyelalamikia huduma zisizoridhisha kutoka moja ya hospitali zilizopo mkoa wa Dar es Salaam alipokwenda kujifungua.

“Mama huyo alidai kutozwa fedha kwa ajili ya huduma yakujifungua na ndipo akaamua kuwasilisha malalamiko yake kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na wakati akimjibu mama huyo ndugu Chalamila alinukuliwa akisema (toka nje chukua bajaji nenda zako nyumbani kamwambie mmeo achukue visu na mikasi akusaidie kujifungua),” ilibainishwa.

LHRC imeeleza kusikitishwa na kufadhaishwa na kauli hiyo inayotweza na kufedhehesha utu wa Mwanamke na misingi ya utawala bora kwani Afya ya uzazi ni haki ya kikatiba kama ilivyoanishwa katika ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na mikataba ya Kikanda na Kimataifa ambayoTanzania ni nchi mwanachama.

Kwa mujibu wa ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya1977, LHRC imearifu kuwa, viongozi wa umma wanawajibika kwa umma ambao ndiyo wenye dhamana ya Serikali na si kutoa kauli za kuwakebehi kwani si mara ya kwanza kwa Chalamila kutoa kauli zenye mtazamo wakutweza utu, kudhalilisha au kukebehi wananchi hadharani.

“Tunakemea vikali kauli hii na kuwaasa viongozi wa umma kuwa na hadhari pindi wanapotoa matamshi yao kwa wananchi. Hivyo, LHRC inatoa wito ufuatao, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan achukue hatua za kinidhamu dhidi ya ndugu Chalamila. 2. Viongozi wote wa umma kuzingatia utu na kutoa matamshi yenye staha na yenye kuonyesha uwajibikaji wao kwa wananchi kama ilivyoanishwa katika ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania 1977,

“3. Sekretariati ya maadili ya viongozi wa umma imuite na kumhoji nduguChalamila kama hatua za kinidhamu hazitachukuliwa dhidi yake.4. Kuboreshwa kwa mitaala ya ufundishaji katika vyuo vya kada ya afyahasa katika eneo la utoaji wa huduma na matumizi ya lugha zenyestaha na kujali,” alibainisha Dkt. Anna Henga kupitia taarifa hiyo.

 

 

BUNGENI: Bilioni 1.8 zatengwa kukarabati taa za Barabarani Nchini
Picha: Rais Samia katika picha ya pamoja na Viongozi wa Afrika