Johansen Buberwa – Kagera.
Wizara ya afya imetangaza kuwa hakuna visa vipya vya wahisiwa wa maambukizi ya virusi vya ugonjwa Marburg nchini, huku idadi ya vifo vikiongezeka na kufikia eatu wawili ambapo 22 waliopimwa awali wamekutwa na ugonjwa wa Malaria.
Naibu waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel akizungumza Mkoani Kagera akiwa Wilayani Biharamulo amesema, hakuna visa vipya vya maambukizi ya virusi hivyo vya MVD)l, tofauti na ilivyotangazwa awali.
Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, SACP Advela Burimba amesema mpaka sasa Wananchi wanaendelea kupatiwa elimu ambapo kaya 10,593 zimetembelewa na kuelimishwa tangu Serikali ilipotangaza uwepo wa virusi hivyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma ya Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Ntuli Kapologwe amesema watu 281 waliohisiwa kuchangamana na Mgonjwa Marburg wanaendelea vyema.
“Kwa waliowekwa karantini watu 145 wameruhusiwa na 92 bado wanaendelea kumaliza siku 21 za uanglizi huku 44 kati ya walioruhusiwa wakifuatiliwa majumbani na kifo cha mtu mmoja kikitokea na kufanya idadi ya waliofariki kuwa wawili,” alisema.