Serikali imejikita katika kuhakikisha inapunguza bei ya gesi ya mitungi ya kupikia (LPG) Nchini ikiwa ni kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034.
Akizungumza hayo Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga Leo Januari 29, 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum Maryam Mwinyi ambapo aliuliza ,Serikali ina Mkakati gani wa kupunguza bei ya gesi ya matumizi ya nyumbani kwa kuwa Wananchi wengi wamepata mwamko.
Amesema, “Serikali inaendelea na utoaji wa ruzuku ya asilimia 20 hadi 50 ya bei ya mitungu ya gesi ya LPG kwa watumiaji wa mwisho ,na pia Serikali itaendelea kuja na mikakati mingine ili kuhakikisha bei ya gesi inapungua.”
Hata hivyo amesema Serikali imeanza mazungumzo na makampuni ya (LPG) ili kuhakikisha wanapata maeneo yote ili Wananchi wakitaka kujaza gesi wajaze gesi kwenye mitungi kwa urahisi.
“Tunaendelea na mikakati hii, na mpaka sasa tumefikia hatua nzuri tumebakiza miezi sita ya utekelezaji wa mkakati huo, niwahakikishie Watanzania kilakitu kitakuwa Sawa, na mtaweza kujaza gesi kwa huaraka zaidi,” amesema Kapinga
Vilevile akijibu swali la Mbunge huyo kuhusiana na vituo vya kujaza gesi kwenye gari ambapo amesema, “kwasasa Serikali inaendelea na ujenzi wa vituo mbalimbali na kwa Dar es salaam tunaujenzi wa vituo vitatu ambavyo tunavijenga kwaajili ya kupunguza foleni ambayo ipo katika vituo vya CNG.”
“Lakini kwakushirikiana na Sekta binafsi tunavyo vituo vingine ambavyo tunavijenga, lakini kupitia shirika letu la maendeleo ya petroli tunanunua vilevile magari ya kuamishika kwaajili ya kuhakikisha barabara zote kuanzia kutokea Dar hadi Morogoro hadi Dodoma kuna vituo hivi kwaajili ya kurahisishia Wananchi wanaotaka gesi kwenye magari,” alisema Kapinga.