Klabu ya Simba imeendelea na mazoezi makali kuelekea mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Tabora United utakaopigwa tarehe 02 Februari Dimba la Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora. Mchezo huo ni muhimu kwa miamba hiyo ya soka kuelekea mbio za ubingwa msimu huu.

Msimu huu wa 2024/25 Tabora si timu ya kubeza kutokana na kuwashangaza wengi kwenye michezo mitatu migumu dhidi ya timu tatu zinazoshikilia nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi ya NBC wakishinda 3-1 dhidi ya Yanga Afrika na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC sare ya mabao 2-2 dhidi ya Singida Black Stars.

Ubabe wa matokeo umekuwa tishio kwa wapinzani na hasa kuelekea mchezo wa raundi ya pili dhidi ya Simba. Mchezo wa kwanza uliopigwa agosti 18 2024 dimba la KMC COMPLEX, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na baada ya mchezo Tabora United walilalamikia uchelewaji wa leseni za wachezaji wa kigeni waliokosekana katika mchezo huo ,Kwa sasa wachezaji hao wameshapata leseni na wameonyesha uwezo  mkubwa wakiisaidia Tabora kushinda michezo 7 sare 4 na kufungwa 4 huku wakishika nafasi ya 5 wakiwa na alama 25 kwenye michezo 15.

Ni kweli Ali Hassan Mwinyi hatoki mtu?

Tabora wanaamini kikosi chao kina uwezo mkubwa wa kushinda mchezo huo na kurejesha heshima ya mkoa wao, Klabu hiyo yenye msemaji machachari Dada Christina Mwagala wamejigamba kwamba iwe jua iwe mvua basi mnyama hatoki salama Ali Hassan Mwinyi,Tabora inajivunia umahili wa wachezaji wake na sapoti kubwa ya mashabiki na viongozi mbalimbali .

Baadhi ya wadau mkoani humo wameahidi kutoa shilingi milioni 50 kwa wachezaji endapo timu itapata matokeo dhidi ya Simba hivyo mchezo lazima uwe mgumu.

Mipango ya Simba kwa mwezi Februari 

Klabu ya Simba kwa sasa inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 40 kwenye mechi 15 walizocheza raaundi ya kwanza. Simba wana mechi 16 raundi hii ya pili na matokeo chanya kwenye mechi hizo yatawahakikisha ubingwa kwa msimu 2024/25. Mwezi Februari Simba anamichezo 6 ya ligi kuu na anapaswa kushinda yote ili kupunguza makali mwezi Machi atakaporejea kushiriki kombe la shirikisho hatua za robo fainali.

2 Februari Simba atakuwa ugenini dhidi ya Tabora United ,Tarehe 6 atakuwa ugenini Mkoani Singida dhidi ya Singida Black Stars,Tarehe 11 Februari atakuwa dimba la nyumbani KMC Complex dhidi ya Tanzania Prisons ,Tarehe 15 Februari atawakaribisha Dodoma jiji KMC cOMPLEX ,Tarehe 19 Februari  atakuwa ugenini dhidi ya Namungo FC na tarehe 24 Februari atawakaribisha Azam FC dimba la Nyumbani.

Kama Simba atashinda michezo hii yote atavuna alama 18 na atafikisha jumla ya alama 58 hii itamfanya aweze  kuendelea kuongoza msimamo wa ligi.Swali ni je wataweza kuzikusanya alama zote 18 mwezi Februari?

Yanga wakishinda mechi hizi 7 Simba wasahau Ubingwa msimu huu
Wanigeria wayapigia hesabu mabilioni ya Victor Boniface