Ligi kuu ya NBC inarejea tena uwanjani kukamilisha mzunguko wa pili wa msimu wa 2024/25. Mabingwa watetezi Young Africans na wao wamo kwenye orodha ya kuendeleza gurudumu la ligi hiyo kwa mwezi Februari. Klabu hiyo chini ya Kocha Saed Ramovic imejipambanua vyema msimu huu kwa kuibuka na ushindi wa mechi 13 na kupoteza mechi 2 tu kati ya 15 walizocheza wakijikusanyia alama 39.
Mwezi Februari Yanga wana kibarua kigumu wakitakiwa kucheza mechi 7 ndani ya siku ya 28 sawa na uwiano wa mchezo mmoja kila baada ya siku nne. Kama Yanga watashinda michezo yote 7 watavuna alama 21 na kufikisha alama 60 hivyo kuongoza msimamo wa ligi na kupunguza presha kuunyatia ubingwa wa msimu huu.
Kwa ratiba hii Yanga ataweza kuibuka na Ushindi kila mchezo ?
Tarehe 1 Januari Yanga watawakaribisha Kagera sugar dimba la KMC complex na Tarehe 5 watawakaribisha Ken Gold katika Dimba hilo.Tarehe 10 Januari Yanga watakuwa ugenini Dimba la Meja General Isamuyo kumenyana na JKT Tanzania. Tarehe 14 Januari Yanga watakaribishwa tena dimba la KMC cOMPLEX dhidi ya wenyeji KMC .Tarehe 17 Yanga watawakaribisha Singida Black Stars dimba la KMC Complex na tarehe 23 watasafiri mpaka kigoma kukabiliana na Mashujaa FC . Tarehe 28 watakuwa ugenini jijini mwanza kupambana na Pamba Jiji.
Ramovic na maajabu yake Yanga
Tarehe 15 Novemba 2024 Yanga walitangaza rasmi kumpa kazi kocha Saed Ramovic ,Wengi walimbeza kutokana na rekodi mbaya aliyoiweka nchini Afrika Kusini alipokuwa klabu ya ……..Mambo yamekuwa ni tofauti na matarajio ya Wengi.Kocha huyo kwa sasa amegeuka kuwa nuru ndani ya Yanga akiiongoza timu hiyo katika michezo 12 ya mashindano mbalimbali akishinda michezo 7 sare 2 na vipigo vitatu.
Kocha huyo amekuwa na cheche kwenye mechi zote tano za ligi kuu ya NBC akiibuka na ushindi dhidi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo, Ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mashujaa,Ushindi wa 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons ,Ushindi wa 4-0 dhidi ya Dodoma jiji,ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Singida Black Stars na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Copco Kombe la CRDB .
Kwa Tathimini ya mechi 6 za Ligi kuu na Kombe la FA kocha huyo ameshinda mechi zote akifunga jumla ya mabao 23 akiruhusu nyavu zake kutikiswa mara mbili pekee. Rekodi hiyo ni muhimu kuzingatiwa wakati huu ambao Saed Ramovic atawaongoza wananchi katika mechi 7 za Ligi kuu kisha mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa machi 8.