Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Manyaram imesema imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi mil. 3.3 Wilayani Mbulu, fedha ambazo zilifanyiwa ubadhirifu na aliyekuwa mratibu wa chanjo ya surua rubella mwaka 2014.

Akizungumza na Wanahabari Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Bahati  Haule amesema Mratibu huyo alifanya ubadhirifu wa fedha zilizopaswa kulipia gharama za chakula cha washiriki 435 wa semina ya watoa huduma ya utoaji chanjo kwa kughushi risiti za marejesho.

Aidha, mratibu huyo alimwaminisha mwajiri wake ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwamba ametumia kiasi cha shilingi 6,525,000 wakati akijua ya kwamba Mzabuni aliyefanya huduma hiyo alilipwa jumla ya Shilingi 3,225,000 na hivyo kumwezesha kujipatia kiasi cha Shilingi Milioni 3,300,000 kwa njia za udanganyifu.

Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Mbulu iliweza kufanya uchunguzi na kubaini na kuthibitisha udanganyifu huo na Desemba 2024 mshatakiva alirudisha fedha hizo pamoja na kuchukuliwa hatua nyingine za kinidhamu.

Hata hivyo, TAKUKURU Manyara kwa kipindi cha mwezi Octoba hadi Desemba 2024, imefuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ishirini 20 inayogharimu jumla ya shilingi 9,765, 514, 213.

Kwa upande wa uchunguzi, TAKUKURU mkoa wa Manyara imepokea malalamiko 98 kutoka sekta mbalimbali ambapo malalamiko 70 yalihusu rushwa na yameshughulikiwa kwa mujibu wa Sheria kwa kuanzisha uchunguzi wa tuhuma hizo.

Polisi yathihitisha vifo vya Watu wawili Moro
Utekelezaji Mradi wa Maji kuvinufaisha Vijiji sita - Kundo