Kiongozi wa kisiasa wa kundi la waasi la M23 Corneille Nangaa wanaoungwa mkono na Rwanda ambao waliteka mji mkubwa wa mashariki mwa Kongo Goma, amesema kazi iliyobaki ni kuingia Kinshasa.
Nangaa, alitangaza nia yake hiyo mapema Januari 30, 2025 akisema sasa wanaelekea mji mkuu wa Kinshasa, kwa lengo la kuipindua serikali ya Rais Félix Tshisekedi ambaye naye alitoa wito kwa Vijana kujiunga na Jeshi ili kuingia kwenye mapambano.
Ikumbukwe kuwa Waziri wa Ulinzi wa Kongo, Guy Kabombo Muadiamvita alitoa maagizo kuwa mipango ya mazungumzo yoyote na waasi isitishwe.
“Tutakaa hapa Kongo na kupigana. Ikiwa hatutaishi hapa, basi tutaishi wafu hapa,” alisema Muadiamvita, mshirika wa karibu wa rais Tshisekedi.
Kwabupande wake Rais Tshisekedi amesema hatakubali kushindwa kwa waasi na aliwataka wananchi wa mashariki mwa nchi yenye rasilimali nyingi kukataa kukubali kutekwa kwa maeneo zaidi na wapiganaji hao.