Wadau wa zao la Chai, wameshauriwa na Bodi ya Chai Nchini (TBT), kuchangamkia fursa ya masoko ya Chai kwani tayari imeweka mikakati na kuongeza uzalishaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania (TBT), Beatrice Banzi ameyasema hayo wakati wa kikao na wadau wa zao la Chai lengo kubwa lilikuwa kujadili namna ya kuongeza uzalishaji wenye ubora.

Amesema, changamoto zinazo likabili zao hilo ni Umeme kukatika mara kwa mara pamoja na miundombinu ya barabara, na kwamba ni lazima Serikali na Sekta binafsi wakae kujadili ni jinsi gani wanaweza kuokoa zao hilo.
Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbali ikiwemo Wizara ya Kilimo, Bodi ya Chai, Tantrade, Bandari na Ushirika na kwa pamoja walipanga mikakati ya ni jinsi gani wanaweza kufikia malengo yao waliojiwekea ya kuendeleza zao la chai kwa muda wa miaka 10 kutoka 2024 mpaka 2034.