Watu watatu wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Rav4 kugongana uso kwa uso na basi la abiria kampuni ya Esther Luxury lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es Salaam.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mdawi, Wilaya ya Moshi huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni dereva wa gari dogo kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.

Amesema, “ajali imetokea leo asubuhi eneo la Mdawi, watu watatu waliokuwa kwenye gari dogo aina ya Toyota Rav4 wamefariki dunia baada ya gari hilo kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Esther Luxury lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es Salaam.”

Wakisimulia tukio hilo, baadhi ya mashuhuda wamesema Basi jingine lilikuwa likiovateki na liliongozana na gari dogo, kisha wakati yakijaribu kurudi katika upande husika ghafla basi la Esther lilikutana uso kwa uso na Rav 4 na kupelekea tukio hilo.

Hata hivyo, Kamanda Mkomagi amesema hakuna majeruhi kwenye basi hilo, na mili ya marehemu waliokuwa kwenye gari dogo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi.

Maboresho ya sera kuondoa changamoto ukosefu wa Maji
Wahimizwa kuchangamkia fusra soko la Chai