Mpango wa Manchester United kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich Mathys Tel watibuka huku Arsenal wakisubiri pembeni, beki wa Chelsea Axel Disasi anawindwa naye Joao Felix anasakwa na AC Milan na Aston Villa.
Mshambuliaji wa Ufaransa Mathys Tel, 19, anataka kujiunga na Manchester United lakini mazungumzo ya kufanikisha azama hiyo na Bayern Munich yametibuka kwa sasa, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikitaka aondoke uhamisho wa kudumu. (Sky Germany)
Manchester United wanamtaka Tel, lakini mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Christopher Nkunku, 27, ni chaguo jingine katika siku ya mwisho. (ESPN)
Arsenal wanasubiri kwa hamu baada ya ofa mbili zilizowasilishwa na United kumsajili Tel kukataliwa siku ya Jumapili. (Mail)
Tottenham wamekubali Chelsea kumsajili mkataba wa mkopo na mlinzi Axel Disasi, 26, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anataka kuhamia Aston Villa. (Fabrizio Romano)
Beki wa kushoto wa Chelsea na England Ben Chilwell, 28, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu ya Crystal Palace, kabla ya kuhamia klabu hiyo kwa mkopo siku ya mwisho wa uhamisho wa wachezaji. (Telegraph – usajili unahitajika)
Newcastle itamruhusu mlinzi wa Uingereza Lloyd Kelly, 26, kuelekea Juventus katika mkataba ambao utafanywa wa kudumu msimu wa joto. (Mail)
Joao Felix anatarajia kuondoka Chelsea siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji huku klabu za AC Milan na Aston Villa zikiwa na nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 25. (Sky Germany)
Manchester United wamejitosa kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Ipswich na England wa Chini ya miaka 21 Liam Delap, 21, ambaye pia amekuwa akihusishwa na nklabu ya Tottenham. (Express)
Ajax haitamruhusu kiungo wa Uingereza Jordan Henderson, 34, kuhamia Monaco kipindi hiki cha uhamisho wa wachezaji. (Mail)
Everton wanashughulikia mpango wa kumsajili beki wa kushoto wa Rennes na Ufaransa Adrien Truffert, 23. (Mail)
Mkufunzi wa Crystal Palace Oliver Glasner anataka kumsajili kiungo wa AC Milan na Serbia Strahinja Pavlovic, 23, kwa mkataba wa pauni milioni 25. (Sun)
Kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya Italia Jorginho, 33, anakaribia kufikia mkataba wa kujiunga na klabu ya Brazil Flamengo msimu wa joto. (Sky Italy, via Sky Sports)
Spurs wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Lorient Mfaransa Eli Junior Kroupi, 18, ambaye pia anawindwa na Chelsea na West Ham. (Football Insider)
Brighton wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa PAOK wa Ugiriki Stefanos Tzimas, 19, ambaye Nurnberg yuko kwa mkopo . (Sky Sports)